Utajuaje kama simu yako imehackiwa na usitishaje? Makala hii itakusaidia jinsi ya kujua nani amekuck na utatoaje hiyo hack.
Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, usalama wa simu na namba ya simu ni muhimu sana. Mtu akipata ufikiaji wa namba yako, anaweza kuhamisha simu zako, kusoma ujumbe wako, au hata kutumia taarifa zako kwa matumizi mabaya. Kwa bahati nzuri, Kujua namba yako ya simu ikiwa imehacked au kuwepo kwa mtumiaji mwingine asiyefaa kunatumia nambari yako au simu yako kuna njia kadhaa zinazoweza kusaidia. Njia rahisi ni kutumia misimbo maalum (USSD codes) ambayo hutumwa kwa simu yako kuangalia kama mawasiliano yako yametumwa kuhamishwa kwa namba nyingine bila idhini yako.
Njia za kufuatilia kama namba yako au simu imehacked ni kama ifuatavyo:
Piga *#61# kwa simu yako.
Kazi yake:
-
Inaonyesha kama simu za kuingia, SMS, au maonyesho (notifications) vinaelekezwa kwa namba nyingine.
-
Ukiona maneno kama “FORWARDED”, hiyo ni ishara kuwa mawasiliano yako yanaweza kuwa yanapelekwa kwa mtu mwingine.
-
Ukiambiwa “NOT FORWARDED”, basi hakuna tatizo.
Piga *#21#
Kazi yake:
-
Inakuonyesha kama simu zako, SMS, au data nyingine zote zinaweza kuhamishiwa kwa namba tofauti bila idhini yako.
Hii ni njia nzuri ya kugundua udukuzi wa kiwango cha juu wa kusikilizwa au kufuatiliwa
Piga *#62#
Kazi yake:
-
Inaonyesha namba ambayo simu yako ina-forward mawasiliano wakati imezima, haina mtandao, au uko nje ya coverage.
-
Ikiwa namba unayoona si yako, kuna uwezekano wa udukuzi.
Kuzuia au kusimamisha forwarding yoyote – ##21#
Ili kuzuia mtu kuendelea kutumia namba yako bila idhini, piga ##21# ambayo itafuta au kuzima uhamisho wowote wa simu au ujumbe unaoendelea kufanywa
Kazi yake:
-
Hufuta na kuzima aina yoyote ya call forwarding kwenye simu yako.
-
Ni muhimu sana ukishuku kuwa mtu amekuwa akipokea simu au ujumbe wako.
Piga *#06# kuona namba ya IMEI ya simu yako.
Kazi yake:
-
Inaonyesha namba ya kipekee ya simu (IMEI).
-
Haioneshi kama umehacked, lakini IMEI ni muhimu kwa:
-
Kufuatilia simu ikipotea
-
Kuzuia simu isiendelee kutumika na mhacker
-
Mambo ya Kufanya Ukishuku Namba Yako Imehacked
- Ondoa apps usizozijua
- Rekisha upya neno siri la akaunti zako (WhatsApp, Gmail, n.k.)
- Weka programu ya usalama au antivirus kwenye simu
- Wasiliana na kampuni ya simu (Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel n.k.)
- Futa call forwarding kwa kutumia ##21#
Kwa ujumla, ikiwa unahisi simu yako imehacked, au mtu anaingia kwenye simu au namba yako bila idhini, kutumia misimbo hii inapatikana kwenye simu yako itakusaidia kugundua na kuzuia shughuli hiyo kwa urahisi. Pia ni muhimu kuangalia matumizi ya data, maombi yasiyo ya kawaida, na kufuta apps zisizohitajika ambazo zinaweza kumsaidia mtu kuingilia simu yako.
Hizi ni baadhi ya hatua rahisi unazoweza kuchukua mwenyewe ili kujua na kugundua kama namba yako au simu yako imehacked.