Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo kuomba nafasi mpya za ajira serikalini kwa mwezi Oktoba 2025.
Kuhusu Sekretarieti ya Ajira (PSRS)
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu cha 29(1). Taasisi hii imepewa jukumu maalum la kuratibu na kusimamia mchakato wa ajira katika taasisi za umma kwa kuzingatia uwazi, usawa, haki na weledi.
PSRS inalenga kuwa kitovu bora cha kutoa huduma za ajira katika ukanda wa Afrika Mashariki. Dhamira yake ni kuhakikisha ajira serikalini zinatangazwa na kushindaniwa kwa misingi ya uwezo na merit, huku ikitumia mifumo ya kisasa ya usaili na usimamizi wa rasilimali watu.
Sekretarieti hii ni mwajiri usiot discriminate na inatoa fursa sawa kwa waombaji wote wenye sifa stahiki.
Maombi ya Ajira
Waombaji wanaotaka kuomba nafasi hizi wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal. Kabla ya kuomba, hakikisha umefanya yafuatayo:
-
Kusahihisha na kukamilisha taarifa zako binafsi kwenye akaunti yako ya Ajira Portal
-
Kuhakikisha Namba ya NIDA (NIN) imejazwa kikamilifu
-
Kuhakikisha taarifa za elimu na vyeti zimewekwa kwenye sehemu husika kwa usahihi
Jinsi ya Kufuatilia Maombi Yako
Baada ya kuwasilisha maombi:
-
Tembelea sehemu ya My Application ndani ya akaunti yako ya Ajira Portal kuona hali ya ombi lako
-
Utajulishwa kama umefanikiwa kuitwa kwenye usaili au sababu za kutokuitwa
Muhimu
Tazama nafasi mpya za ajira serikalini zilizotangazwa mwezi huu kupitia ukurasa rasmi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Ajira Portal Login: Bonyeza hapa kuingia
Maelezo ya kazi na maombi rasmi: Bonyeza hapa kuona nafasi zote